UONGOZI wa Mwadui FC ya Shinyanga kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Ramadhan Kilao amesema timu yake imekuwa ikiendelea na mazoezi ya wachezaji wake kujiweka fiti ili ligi itakaporejea wote wawe kwenye kiwango bora kwa kuwa hawako vizuri katika msimamo wa Ligi Kuu Bara msimu huu.
                        
Kilao amesema: "Wachezaji wetu kiukweli wamekuwa wakiendelea na mazoezi binafsi nyumbani, kocha wetu Khalied Adam aliweka utaratibu wa kila mchezaji kufanya mazoezi binafsi.

“Lengo ikiwa ni wachezaji wetu waendelee kuwa fiti na hilo tumelifanikisha, kwani karibia kila siku tunapata ripoti ya kocha wetu kwa namna wanavyoendelea na mazoezi yao. 

"Kocha wetu kwa sasa yuko likizo na tumefanya hivyo kwa sababu hata kambini hatuna wachezaji, tumewapumzisha kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

“Pamoja na hivyo, huko aliko kwa kushirikiana na benchi lake la ufundi tunapata taarifa zote na hata wachezaji wanaougua tunatoa matibabu kwao ili waweze kuendelea kujifua."

Aidha, Kilao amesisitiza kuwa malengo ya timu yake ni kumaliza ligi ikiwa miongoni mwa timu 10 bora katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

“Ukiangalia namna tulivyoanza ligi tulianza kwa kusuasua lakini kwa sasa tumeshagundua wapi tulikosea tunajipanga ili tuweze kufanya vizuri na kutimiza malengo," alisema katibu huyo. 

Mwadui FC ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi  34 baada ya kucheza mechi 28.

Ilikuwa timu ya kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara kuitungua Simba kwenye mchezo wao uliochezwa Shinyanga kupitia kwa Gerald Mdamu.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.