SARAKASI za usajili wa kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama imezua sura mpya baada ya kuelezwa kuwa, Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ kuwapigia simu viongozi wa Yanga ili kujua juu ya jambo hilo.

Habari kutoka chanzo cha kuaminika kutoka Yanga zimeliamba dawati la Spoti Xtra kuwa, baada ya Yanga kuendelea kutamba kwamba imefanya mazungumzo na Chama ili kumsajili mwishoni mwa msimu huu, Simba wameanza kuingiwa na wasiwasi hali iliyomfanya Mo kuwasiliana na viongozi wa Yanga.


Ishu ya Chama kutakiwa na Yanga imekuja siku chache baada ya mabosi wa Yanga kupitia wadhamini wao, GSM kusema kuwa hawashindwi kuipata saini ya mchezaji yeyote kwani wana uwezo wa kumchukua yule wanayemtaka.


Chama ambaye hivi karibuni alisema kwamba taarifa za yeye kutakiwa na Yanga si za kweli, bado ana mkataba na Simba hadi 2021 ambapo alijiunga nayo msimu uliopita akitokea Power Dynamos ya Zambia.

“Viongozi wa Simba wana wasiwasi mkubwa wa kumpoteza Chama, hii ni baada ya Yanga kuja juu kutangaza kwamba wanakaribia kumsajili na tayari wamefanya naye mazungumzo.


“Hali hiyo imemfanya hata Mo kumpigia mmoja wa viongozi wa Yanga kutaka kufahamu ishu hiyo imekaaje wakati wao wanajua bado Chama wana mkataba naye,” kilisema chanzo hicho.


Ikumbukwe kuwa, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, ndiye aliyekuwa akisikika sana kuzungumzia ishu hiyo ya Chama kabla ya kuibuka tena na kuweka wazi kwamba alikuwa akifanya utani kama ambavyo Simba walivyokuwa wakiwasumbua kwa kiungo wao Papy Tshishimbi.


Mwakalebela amesema:-“Ukizungumzia Yanga unazungumzia taasisi kubwa, kwa ishu ya Chama mengi yamezungumzwa ila nikwambie kitu ninajua utaratibu wote kuhusu masuala ya usajili, hivyo kwa kuwa niliongea awali bado ninasisitiza kuomba radhi lakini mambo yakikamilika kila kitu kitakuwa sawa.


”Alipoulizwa juu ya kama kweli walikuwa wakimuhitaji Chama na ana maoni gani wakati huu ambao Simba wameonekana kupaniki, Mwakalebela alisema: “Ishu hiyo siwezi kuizungumzia sana kwa sababu kuna kama siasa, hebu angalia kwa nini tuliposema tumezungumza na Chama wao walipaniki wakati wanadai wana mkataba naye mrefu, kiukweli iliwashtua mpaka Mo akanipigia simu.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.