KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, Etienne Ndayiragije amesema kuwa wachezaji wanapaswa wasikae bila kufanya mazoezi wakati huu wakiwa hawachezi.

Ligi nyingi zimesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo wachezaji wamerejea nyumbani kuchukua tahadhari.

Ndayiragije amesema:"Wakati huu kwa kila mchezaji ni muhimu kufanya mazoezi ambayo yatamfanya awe bora , iwapo atapuuzia ni rahisi kiwango chake kushuka.

"Aina ya mazoezi itategemea pia na aina ya mechi ambazo alitoka kucheza kabla ligi hazijasimamishwa, ni matumaini yangu kwamba wamepewa program na makocha wao hivyo ni lazima wafuate,". 

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.