INAELEZWA kuwa bosi mmoja wa GSM anatarajiwa kupanda ndege hadi nchini DR Congo kwenda kumalizana na winga wa AS Vita, Tuisila Kisinda mwenye miaka 20 akimudu kucheza kiungo wa pembeni (winga).
Winga huyo inaelezwa aliwahi kuwaniwa na Simba, Desemba, mwaka jana lakini dili halikufanikiwa.
Taarifa za uhakika zinasema kuwa Kisinda anakuja Yanga kufuatia mapendekezo ya kocha Luc Eymael, ambaye aliagiza kusajiliwa kwa winga mmoja wa kimataifa mwenye uwezo wa kucheza soka la spidi.
Chanzo hicho kilisema: “Kuna kiongozi mmoja wa GSM, anatarajia kusafiri kuelekea Congo, kwenda kumalizana na Kisinda ambaye anacheza AS Vita, kama ambavyo unajua kuwa kocha amependekeza kusajiliwa kwa wachezaji wanne wa kimataifa, hivyo huyo naye ni mmoja wao.”
Msemaji wa Yanga, Hassan Bumbuli amefungukia ishu hiyo kwa kusema: “Wengi wanazungumzia suala la usajili licha ya kuwa muda wa usajili bado, lakini ni kweli kocha alitoa mapendekezo ya kusajiliwa kwa wachezaji wanne wa kimataifa mapema kabla ya pre-seasons.
“Nafasi alizopendekeza ni mshambuliaji mmoja, winga, kiungo na beki, na tayari GSM ambao wanasimamia masuala ya usajili wanaendelea na mazungumzo na wachezaji hao.
“Kwa hiyo muda ukifika tutasema ni akina nani na wanatoka nchi gani, kwa sababu kwa sasa itakuwa siyo busara kutaja majina ya wachezaji hao kwa sababu mambo bado, kwa hiyo muda ukifi ka tutawaweka wazi kwa wanahabari,” alisema Bumbuli.
Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka Brand Chapa GSM, Mhandisi Hersi Said ambaye ndiye mara nyingi anahusika na ishu ya usajili Yanga, ili atoe neno juu ya ishu hiyo ambapo alitoa jibu fupi kwa kusema: “Bado, yote katika hayo.”
Chanzo: Championi
Post a Comment