STAA wa zamani wa Klabu ya Barcelona, Xavi Hernandez amefunguka kuwa kwa sasa ni wakati sahihi kwa yeye kurejea na kwenda kuinoa klabu yake hiyo ya zamani.
Barca ilitaka kumchukua staa huyu awali kama mbadala wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Ernesto Valverde lakini ikashindikana na timu kwa sasa ipo chini Quique Setien.
Xavi baada ya kustaafu soka kwa sasa ni kocha ambaye anakinoa kikosi cha Al Sadd nchini Qatar na anafurahia maisha huko.
Staa huyo alisema kwa sasa anatamani kuona siku moja anarejea katika klabu yake na kwenda kuifundisha hii ni baada ya kuwa vizuri.
Xavi alisema: “Nimeshajipima mwenyewe kama kocha tayari kwamba sasa naweza kupambana na ndoto yangu ya kwenda kuifundisha Barcelona naona huenda ikatimia siku moja kutokana na hili ambalo naliamini mimi.
" Nimeshasema mara nyingi nimekuwa nikizungumza kuwa nataka kurejea nyumbani na Barcelona pale kwangu ni nyumbani naamini wakati utafika tu.
“Nipo hapa Qatar ambapo nimejifunza mambo mengi ambayo yanazidi kunijenga katika kazi yangu na pia nafurahia maisha ya hapa pia.
“Ila suala ya kuifundisha klabu kama Barcelona ni kitu kikubwa ambacho natakiwa kufikiria kwa umakini mkubwa kabisa bila tatizo.
“Natakiwa kujipanga na kujiandaa ili siku au wakati ukifika nisipate shida kwenye hilo,” alisema Xavi.
Post a Comment