IMEZIDI kuwa tamu sasa promosheni namba moja Bongo ya Chomoka na Gari inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publisher wazalishaji wa magazeti ikiwa ni pamoja na Championi na SpotiXtra ambapo washindi watatu leo wanakabidhiwa zawadi zao.
Ofisa Masoko wa Global Publisher, Anthony Adam amesema kuwa baada ya kucheza droo ya kwanza kwa mafanikio Machi 25 bado promosheni inaendelea na wasomaji wanapaswa kuendelea kutuma kuponi zaidi.
“Tulipata washindi watatu kutoka mikoa mitatu tofauti hiyo inaonyesha kwamba tupo sawa na hakuna mshindi aliyepangwa, zawadi zao za Smartphone mpya kabisa watakabidhiwa kesho(leo).
“Kwa wale wa mikoani ambao ni wawili, Swaleh Mohamed wa Tanga na Yesse Daniel ambaye ni mkazi wa Moshi hawa watakwenda kwa mawakala wa mjini kuchukua zawadi zao tayari zimefika na uhakika ni asilimia kubwa kwani hatubahatishi, huku Neema Chuma wa Dar yeye atakabidhiwa zawadi yake makao makuu ya Global Publisher, Sinza” alisema Adam.
Kushiriki promosheni hii ambayo inaendelea ni rahisi, nunua gazeti la Championi kwa 800 ama SpotiXtra kwa jero kisha ukurasa wa pili kuna kuponi utajaza na kumpa wakala aliye karibu nawe na unaweza kutuma kwa njia ya Sanduku la Posta bila matatizo. 

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.