WACHEZAJI wa Arsenal, wamekubali kukatwa asilimia 12.5 ya mishahara yao, baada ya kuahidiwa bonasi kubwa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Wachezaji hao watafidia fedha watakazokatwa kwa kila mmoja kulipwa pauni laki moja endapo watafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa ya Ulaya msimu ujao.

Klabu pia, imeahidi kumlipa kila mchezaji bonasi ya pauni laki tano (Sh bilioni 1.4) kama watatwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2021 au pauni laki moja (Sh milioni 287.9) kama wataibuka mabingwa wa Europa League.

Endapo Arsenal itafuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao wa 2020/21, inamaanisha kwamba wachezaji wa timu hiyo fedha zao zinazokatwa hivi sasa zitarudi zote.

Arsenal, imekuwa klabu ya kwanza ya Ligi Kuu England, kukubali mpango wa kukata mishahara kwa wachezaji wake, katika kipindi hiki ambacho klabu nyingi duniani zimeathirika kiuchumi kutokana na janga la Virusi vya Corona

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.