Vilabu vya kandanda Ujerumani vinatumai kurejea dimbani hivi karibuni, hata kama ina maana kucheza mechi bila mashabiki viwanjani.
Hii ni baada ya waziri wa afya Jens Spahn na viongozi wa majimbo kusema kuwa huenda mechi zikaanza kuchezwa tena kuanzia Mei 9. Viongozi wa majimbo ya Bavaria na North Rhein Westphalia wamesema kuwa kama ligi itarejea basi itakuwa bila mashabiki viwanjani.
Ligi Kuu ya Kandanda ya Ujerumani - Bundesliga, kama tu ilivyo kwa ligi nyingine kuu za Ulaya, ilisitishwa tangu katikati ya mwezi machi kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, ambavyo vimewaambukiza zaidi ya watu 143,000 na kuwauwa zaidi ya 4,500 nchini Ujerumani.

Post a Comment