VALENCIA imejipanga kuanza mazoezi yake kama klabu ifikapo, Aprili 13, mwaka huu, licha ya mastaa wake kupata Virusi vya Corona na tayari wengine wamepona.
Mechi yake ya mwisho ilichezwa dhidi ya Atalanta ya Italia nchini Hispania huku wapinzani wao kutoka Italia walishinda na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya nyota wa timu hiyo wataanza mazoezi Aprili 13, mwaka huu.
Mpaka sasa bado tarehe rasmi za La Liga kurejea haijatangazwa.
Post a Comment