IWAPO msimu wa 2019/20 wa Ligi Kuu England ukifutwa, Liverpool inabidi isahau kutwaa ubingwa licha ya kwamba inaongoza ikiwa na pointi 82 kibindoni.

Mamlaka za soka barani Ulaya wameeleza kuwa Kuna uwezekano mkubwa wa msimu huu wa 2019/20 kufutwa ikiwa shughuli za soka hazitarejea hadi kufikia Juni mwaka huu.

Aleksandr Ceferin, Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) amesema kuwa kuna mambo yanaweza kutokea kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Sababu kubwa ya kusimamishwa Ligi ni kupisha na kupunguza maambukizi ya Virusi vya Corona. "Kuna mpango A,B n C ligi zinatarajiwa kurejea katikati ya Mei, ikishindikana hapo inamaanisha kuwa msimu utakuwa umefikia tamati na umepotea.


 "Kuna uwezekano mambo yakiharibika basi kuanza upya msimu ujao tunalifanyia kazi na tutatoa majibu baada ya kulizungumza na wakuu wa Vilabu," amesema Ceferin.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.