THAMANI ya mshambuliaji anayekipiga ndani ya Klabu ya PSG, Kylian ambappe imeripotiwa kuporomoka kwa kasi kwenye soko la wachezaji kutokana na janga la maambukizi ya Virusi vya Corona.
Awali thamani ya nyota huyo raia wa Ufaransa sokoni ilikuwa ni pauni milioni 189 na inatajwa inaweza kushuka zaidi ya hapo kufikia pauni milioni 150.
Cohn Bendit ambaye ni mbunge nchini Ufaransa na mwanachama wa Bunge la Umoja wa Ulaya anaamini kuwa thamani ya Mbappe itashuka zaidi kutokana na mtikisiko wa uchumi uliosababishwa na maambukizi ya Virusi vya Corona ambao anaamini utaathiri pia sekta ya michezo.
Ripoti zinaonyesha kuwa ada za masuala ya usajili kwa wachezaji wengi zimeanza kuporomoka kwa kasi ghafla kutokana na timu nyingi kubana matumizi katika kipindi hiki kigumu cha maambukizi ya Virusi vya Corona.
Post a Comment