KATIBU Mkuu wa Klabu ya Mwadui FC, Ramadhan Kilao amesema kuwa wachezaji wote wamepewa program na Kocha Mkuu Khalied Adam ili kulinda vipaji vyao.
Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa na Serikali kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona hivyo wachezaji wanafanya mazoezi binafsi wakiwa nyumbani.
Kilao amesema:"Wachezaji wapo kwenye mapumziko ya lazima ambapo tumewaambia wachukue tahadhari na waendelee kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona ila wasisahau kufanya mazoezi binafsi.
"Kocha amekuwa akiwafuatilia kwa ukaribu ili kujua namna gani wanaendelea kufanya mazoezi lakini kikubwa ni kuona kwamba wanafuata maelekezo ili ligi itakaporea wawe fiti,".
Mwadui FC ipo nafasi ya 12 ikiwa imecheza mechi 28 ina pointi 34.
Post a Comment