MAPAMBANO lazima yaendelee kwa sasa licha ya kwamba kuna Virusi vya Corona ambavyo vinaitikisa dunia.
Virusi hivi ambavyo vinasababisha ugonjwa wa COVID-19 inabidi tukubali kwanza kwamba vimeleta mtikisiko kwenye ulimwengu wa michezo pamoja na sekta nyingine ambazo zimekuwa zikiathirika pia.
Tunaona kwamba ile burudani ya Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda na pia hata kule kwenye mechi za Ligi Daraja la Kwanza kila kitu kimesimama kwenye familia ya michezo vingi tunakosa.
Nguve kazi inapungua kutokana na vifo ambavyo vintokea ila haina maana kwamba nasi lazima tuwe na hofu kubwa hapana tuamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa hapo baadaye ila tusiwe na hofu ya kupitiliza.
Agizo la Serikali lisipuuziwe kwa kuwa hakuna kiongozi anayependa kuona watu anaowaongoza wanapita kwenyye matatizo ni lazima achukue hatua ili kuwaweka salama watu wake.
Ikumbukwe kuwa Waziri mkuu, Kassim Majaliwa, Machi 17 alizuia masuala yote ya mikusanyiko isiyo ya lazima na kusimamisha shughuli zote za michezo kuanzia Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Wanawake.
Bado hatujatoka huko kwa sasa tunapaswa kuendelea kupambana kwa pamoja kila mmoja kwa wakati wake na hapo ndipo tutaweza kuuthibitisha ule usemi wa kwamba umoja ni nguvu.
Afya ni kitu cha msingi kwa wana familia ya michezo pia kumlinda mwanamichezo mwenzako pia ni muhimu tusichukulie utani kwa sasa.
Tukiachana na masuala ya Corona ambayo nimuhimu kukumbushana hasa kwa nyakati hizi leo ningependa nizungumzie kuhusu mipango ya wachezaji na timu kiujumla.
Tunaona ligi zote zimesimama kwa wakati huu ni muhimu kuchukua tathimini ya wapi ambapo timu ilikuwa ikishindwa kufanya vizuri kisha dawa ianze kutafutwa kwa wakati huu.
Kinachotakiwa kufanya kwa sasa ni kutumia mapumziko haya ya lazima kwa ajili ya kutafuta nguvu mpya ya kumaliza ligi iwapo hali itatengamaa kwani hakuna ambaye anajua kwamba lini ligi itarejea.
Kuna timu ambazo mpaka sasa hazijawa na dira nzuri kutokana na kuwa na matokeo mabovu hivyo muda wao wa kutafuta pale ambapo walikwama mwanzo wa msimu kutafuta majibu ya makosa yao.
Ni ngumu kufanikiwa kwa asilimia kubwa kwa kuwa timu nyingi zimevunja kambi lakini kuna namna itakayowafanya mtambue kwamba kuna sehemu ambayo mlikuwa mnakosea lazima muifanyie kazi.
Kuna makocha ambao walikuwa wanaeleza kuwa wanshindwa kupata matokeo kutokana na wachezaji wao kuchoka hasa kwa kusafiri muda mrefu basi ni muda wa kuwapa wachezaji mapumziko.
Pale ambapo watakuwa na muda mwingi wa kupumzika iawafanya watatue lile tatizo la uchovu na watarudi wakiwa kwenye nguvu mpya na mtazamo mwingine.
Zipo timu nyingine ambazo ushindi wao ulikuwa unategemea baadhi ya wachezaji lakini wameshindwa kufikia malengo kutokana na aina ya mfumo wa kocha, katika hili pia ni lazima kutafuta suluhisho.
Kocha lazima atazame upya aina ya wachezaji alionao ili kuwajenga upya na kuwatengeneza muunganiko mzuri ambao utampa nafasi ya kupata matokeo anayohohitaji.
Muda huu pia ni wakati wa kuwakumbusha wachezaji kwamba muda wa kubaki ndani ya ligi unakaribia kumeguka hivyo lazima wapambane ili kulinda nafasi zao ambazo wapo.
Wasisahau kwamba kuna timu nne ambazozinashuka daraja msimu huu hivyo kushindwa kuchukua tahadhari mapema itakuwa ni hasara kwa timu iwapo itaweza kushuka daraja.
Matokeo mazuri hayaji kimiujiza ama kwa kuongea tambo nyingi kabla ya mechi hakuna kitu kama hicho ni lazima kuwe na mipango na mbinu makini.
Timu ambayo itashindwa kufanya mipango vizuri itarejea na kuonyesha kile kilichokuwa kinafichwa hadharani ambapo kila mmoja atajua kupitia matokeo uwanjani.
Mchezo wa mpira upo wazi kwa kila mmoja kuona kile ambacho mchezaji anakifanya iwapo atashindwa kufanya vizuri inamaanisha kwamba hakujipanga na alikuwa hajui anahitaji nini.
Hakuna ruhusa ya kuzembea kutimiza majukumu kwa mchezaji akiwa ndani ya uwanja pamoja na wakati huu ambapo amepewa program ya kufanya.
Kwa matokeo mazuri ambayo ni furaha ya timu na mashabiki lazima kupanga mpango makini kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi ili kuona wanapata kile wanachostahili.
Endapo ligi itareja tunaingia kwenye dakika za mwisho kumtafuta bingwa mpya ambaye atatwaa taji lake msimu wa 2019/20 ni muhimu pia kulitambua hilo.
Tayari timu nyingi zilikuwa zimecheza mechi nyingi za ligi na ilikuwa ipo mzunguko wa pili ambapo timu nyingi zimebakiwa na mechi 11 na nyingine 10 hivyo ni mua mchache umebaki.
Kwa mechi ambazo zimebaki ni mwendo wa hesabu ka kila timu kuona itavuna nini iwapo itamaliza mechi zake zilizobaki kwa sasa.
Zipo ambazo hazina bahati kwamba hata ikitokea zikashinda mechi zote haina uhakika wa kubaki kwene ligi hii ni hatari.
Changamoto ni lazima ziwepo lakini suluhisho pia ni muhimu kutafutiwa hasa kwa muda huu ambao hauna presha kwenye mechi za ushindani.
Post a Comment