UONGOZI wa Yanga umesema kuwa unawafuatilia kwa karibu nyota wote wanaokipiga ndani ya Ligi Kuu Bara ili waweze kuona namna gani wanaweza kuzipata saini zao ikiwa ni pamoja na Relliats Lusajo na Lukas Kikoti.
Miongoni mwa nyota ambao wanafuatiliwa kwa ukaribu na Yanga ni pamoja na pacha hiyo ya Namungo ambayo imekuwa na muunganiko mzuri.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa Klabu ya Yanga inazifuatilia timu zote ndani ya Bongo ili kuona inapata wachezaji wazuri.
"Yanga inafuatilia wachezaji wote ndani ya Ligi Kuu Bara ili kuona namna gani inaweza kupata saini zao kwani kila timu inahitaji wachezaji makini.
"Kuhusu kupata saini zao kwa sasa hao akina Lusajo, Kikoti ni tetesi tu ila wakati wa usajili ukifika tunaweza kuzungumzia hilo ila kuwafuatilia wachezaji ni jambo la kawaida kwa sasa," amesema.

Post a Comment