WILLIAM Lucian, ‘Gallas’ beki wa kuliwa wa Polisi Tanzania amesema kuwa uongozi wa Polisi Tanzania upo makini kwenye kufuatilia maendeleo ya wachezaji pamoja na kujali maslahi ya wachezaji.
Polisi Tanzania ipo nafasi ya sita ikiwa imecheza mechi 29 kibindoni ina pointi 45 huku ikifunga mabao 29 na safu ya ulinzi imeruhusu mabao 26, kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.
Akizungumza na SpotiXtra, Gallas alisema kuwa katika vitu ambavyo vinaifanya Polisi Tanzania kuwa ndani ya 10 bora ni pamoja na balaa linalofanywa na viongozi kwenye kufuatilia kile ambacho wamekiahidi na kukihitaji.
“Balaa letu tukiwa uwanjani linabebwa na viongozi ambao nao wamekuwa makini kuona kwamba kile wanachokitaka kinatokea hivyo wanajali wachezaji na kutimiza stahiki zao kwa wakati.
“Jambo hilo linatufanya nasi pia kwa wakati huu ambao tupo kwenye haya mapumziko ya lazima kuendeleza utamaduni wetu wa kujali kile ambacho tumeambia na uongozi kwani ni lazima tufuate kwa manufaa yetu na timu,” alisema Gallas

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.