April 2020


MANAHODHA wa Bongo wakati wa kuzinduka na kuendeleza ile vita ya kupambana na adui Corona kwa vitendo ni sasa kwani hakuna muda mwingine ambao tutapata wa kuanza kupambana kwa vitendo.
Hali sio shwari kwenye dunia kwani mtikisiko ambao umepita ni mkubwa hivyo ni lazima  wenye busara ambao ni viongozi watakakoanza kuutuliza mtikisiko wa namna hii wawepo.
Miongoni mwa wanaoweza kuwa mstari wa mbele katika hili ni manahodha wa timu zote Bongo kuanzia zile zinazoshiriki Ligi Kuu Bara mpaka zile za hatua ya ngazi ya vijiji bado ni timu.
Ninatambua kwamba kwenye mitaa pia kuna timu ambazo zina manahodha wao zile ambazo zinapiga mpira wetu wa kitaa tunaziita chandimu bado ni timu pia zinawatoa wachezaji wengi tu.
Kuanzia makapteni wa chandimu ni muda wa kuungana na kuwa na nguvu moja katika mapambano dhidi ya Corona kwani kwa namna moja ama nyingine katika michezo yote pande zote zinatugusa pia.
Enzi zile wakati tunarukaruka kwenye madarasa yaliyojengwa na mababu zetu achana na madarasa ya sasa ambayo mbele kuna ubao mweusi na mwalimu anashika chaki kisha anaandika nawe unagandamizia.
Hapa nazungumzia madarasa yale yaliyokuwa chini ya mwembe, kwa wapenda shule walikuwa wanaichukia mvua kwa kuwa ikinyesha hapo ndio mapumziko yanaanzia.
Sasa wakati ule tulikuwa tunafundishwa kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu ninaaona kwamba iwapo manahodha wote wataungana katika hili itaongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya Corona.
Hebu pata picha namna ambavyo John Bocco wa Simba alivyo na uwezo katika kukiongoza kikosi cha Simba kwa mfano akisema kuwa anaanzisha mfuko ambao wachezaji wote Bongo watatupia hata buku tano hivi kwa ajili ya Corona unadhani nini kitatokea.
Kisha sapoti kubwa ataipokea kutoka kwa mtu wa watu Pappy Tshishimbi nahodha wa Yanga na sapoti pia kwa Relliats Lusajo yule wa Namungo mambo yatakwenda kwa kasi.
Achana na hao yupo mkongwe wao ambaye ana busara pia huyu hapa Juma Kaseja anayekipiga ndani ya KMC unadhani akitoa neno katika hili kwamba kwa yoyote yule ambaye ni mchezaji ajitoe kwa ajili ya kupambana na Virusi vya Corona.
Ngoma itakuwa bado haijapoa kuna Jaccob Massawe yeye anawakilisha Gwambina unadhani atagomea wazo kama hili wakati huu wa mapambano dhidi ya Virusi vya Corona?
Wengi huwa tunawaskia kwenye vyombo vya habari kwamba mnawatazama wale wanaokipiga nje akina Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Mohamed Salah  kwa namna wanavyofanya basi na yale ambayo wanayafanya tuyaige pia.
Tunaona kwamba wenzetu wanaoshiriki Ligi Kuu England kupitia kwa manahodha wameungana na wanaendeleza sapoti kwa ajili ya kupambana na Corona.
Hakuna baya kuiga katika hili ni jambo jema na linapendeza pia hivyo italeta maana ikiwa kutakuwa na mfuko Bongo unaowahusu wachezaji pekee wakiungana na Serikali katika kupambana na Virusi vya Corona.
Tunaona kwamba Serikali imekuwa bega kwa bega kaika masuala yanayohusu michezo na inatoa sapoti kubwa katika kila hatua basi na katika hili tuungane wanafamilia ya michezo ili kushinda kwa pamoja.
Haina maana kwamba wanafamilia ya michezo tupo nyuma  hapana ila kuna mambo ambayo kwa sasa yanatakiwa yafanyike ili kesho itakapofika kila mmoja atambue kwamba alihusika kwa namna gani kupambana na vita hii.
Ni ngumu kuamini kwamba kwa sasa hakuna ambaye hana maumivu katika hili janga ila ni muhimu kutambua kwamba kazi yetu moja kubwa kwa sasa ni kuendelea kupambana mpaka hatua ya mwisho.
Kuwa mabalozi nyumbani na kwa familia pekee bado ni deni kwetu kwa ajili ya wengine na wale ambao wanafuatilia kwa kuonyesha kwamba tupo pamoja na tunajali.
Hakuna mkataba wa kunyoosha mikono wakati huu mapambano lazima yaendelee ili kuona namna gani tutaibuka vifua mbele.
Manahodha wasaidizi nao pia nina amini hamtawaangusha viongozi wenu katika hili la kupambana na Virusi vya Corona.
Mzee wa kumwaga maji Juma Abdul wa Yanga, Mohamed Hussein wa Simba ni wakati wa kuendelea yale mavitu ya uwanjani kwa jamii na kwa vitendo.
Italeta picha nzuri kwamba wakati ule vita inakwishwa nasi pia tunakuwa ni sehemu ya ushindi wa vita hii ambayyo imefanya mambo mengi kusimama.
Kusimama kwa michezo kunatukosesha ule uhondo ambao tulikuwa tumeuzoea hasa kwenda kuona namna ushindani ulivyo na mpaka mshindi anapatikana.
Kwa sasa mambo yamekuwa yakienda kwa kusuasua kutokana na shughuli nyingi kusimama kwani licha ya kwamba bado watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kiasi fulani kuna anguko kwenye suala la ajira za watu binafsi.
Ndugu zetu waliokuwa wakionyesha mechi kwenye vibanda umiza kwa sasa hawana chaguo la kufanya zaidi ya kubadili mipango upya.
Yote kwa yote jukumu ni letu kupambana kwa vitendo mpaka pale tutakaposhinda na kuwa pamoja katika maisha ya kawaida

HALI sio shwari kwa sasa kwa kuwa mambo megi duniani yamesimama na hii inatokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vinaitikisa dunia.
Kwenye kila sekta Corona imegusa na kuweka mtikisiko wake huku maumivu yakiwa ndani ya mioyo ya watu.
Ninaona kabisa mambo yanazidi kuwa magumu katika sekta nyingi lakini haina maana kwamba tunapaswa kukata tamaa hapana ni wakati wa kufanya dua kwa Mungu ili janga hili lipite.
Kila kona wamekuwa na namna yao ya kupambana ili kuchukua tahadhari ambapo kwenye sekta ya michezo ambayo inajumuisha watu wengi asilimia kubwa ligi nyingi zimesimamishwa kwa muda usiojulikana.

Tunaona kuna baadhi ya nchi kama Ubelgiji ligi zao zimefutwa pamoja na ile ya Uholanzi hizi msimu huu hazitaendelea na sababu kubwa ni Corona.
Ujue kuna watu ambao bado wanaichukulia kawaida hili tatizo kiukweli kabisa hili janga ni kubwa na lina balaa lazima tuchukue tahadhari kwa umakini kabisa.
Kila mmoja kwa sasa ni lazima awe balozi wa usalama wa mwenzake ili kuona kwamba kila mmoja anakuwa salama kwa wakati huu ambao upo.
Majirani zetu Kenya, Uganda, Rwanda nao pia wapo kwenye suala la kuchukua tahadhari nasi tusipuuze tufanye hivyo ili kulinda afya zetu na familia pia.
Ligi zote hapa Bongo pia zimesimamishwa hilo lipo wazi na wachezaji wamekosa kucheza kwa muda mrefu haina namna ya kuzuia ni lazima kukubali hali halisi.
Wale ambao wanafikiria hili suala ni jepesi basi kuna ulazima wa kufikiria upya na kuanza kuchukua tahadhari kwa kuwa mambo bado hayajawa shwari.
 Wachezaji kwa sasa wengi wapo majumbani ambapo wanaendelea na program ambazo wamepewa na benchi la ufundi.
Kwa muda huu ni wakati wao kuonyesha kwamba wamepevuka kwa kutimiza yale ambayo wamepewa ili kulinda vipaji vyao.
Kipimo cha wao kuwa peke yao nyumbani ni kufanya mazoezi binafsi na kujisimamia kwa umakini bila kumdanganya mwalimu wao kwa sababu hayupo.
Program zao sasa ambazo wamepewa wanapaswa wazifanye kwa umakini mkubwa bila kukosea kwani ni kazi yao na maisha yao kwa sasa.
Ni wakati wa wachezaji kujipanga wenyewe wakiwa nyumbani na uzuri ni kwamba ratiba inakuwa mikononi mwao wenyewe wanajua namna ya kuipanga kiusawa bila kupangiwa.
Iwapo watashindwa kuwa waaminifu katika kipimo hiki ambacho kimesababishwa na Corona wanaingusha timu jumla pamoja na wao wenyewe kuzidanganya nafsi zao.
Iwapo watakuwa wanafanya mazoezi nyumbani kwa sasa pindi watakaporejea iwe leo ama kesho kwenye mechi za Ligi Kuu Bara mambo yatakuwa wazi na kila mmoja ataona namna ambavyo walikuwa wakijifungia ndani na kufuata zile program walizopewa.
Matokeo yataonekana uwanjani kwani mchezo wa mpira ni namba daima huwa hazidanganyi katika kuleta ukweli wa mambo yale ambayo yamejificha.
Kila mmoja yupo nyumbani kwa wakati huu hilo lipo wazi na hakuna namna ya kumfanya mwalimu awe ndani ya nyumba ya kila mchezaji kutazama kile anachokifanya.
Hivyo leo ligi ikianza itakuwa wazi kwa kila mchezaji ambaye alikuwa anafanya mazoezi ama anarukaruka tu wakati huu wa mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.
Hali hii haipo kwetu pekee hata kwa wenzetu ambao wameendelelea huko Ulaya wanapitia ugumu katika kufuatilia mazoezi ya wachezaji pamoja na lishe.
Hivi karibuni tumeskia Manchester United wao wanatoa somo la masuala ya upishi kupitia mitandao kwa wachezaji wao inatokana na kujali na kuhitaji namna gani wachezaji wao wale lakini bado mambo ni magumu.
Ila teknolojia kule mbele kwa wenzetu inawabeba kwani kuna wakati ambao mwalimu anaweza kufanya na wachezaji mazoezi kupitia kwenye mtandao na kila mmoja akamuona mwalimu na wakapeana maelekezo kwa vitendo.
Muda unavyozidi kwenda hali inakuwa tete kwa sasa hivyo ni jukumu sasa la wachezaji kuona namna gani watalinda vipaji vyao ambavyo vinahitaji kulindwa kwa kufanya mazoezi.
Sisi hatupo sawa na mbele kwamba tuanze kufanya mazoezi ya vitendo kwa mtandao ingawa tunafuatilia sio kwa wepesi ule ambao wenzetu wanapata.
Pia na kwa upande wa miundombinu wachezaji wa nje wanakila kitu ndani utakuta mchezaji nyumbani kwake ana uwanja wa kuchezea mpira, sehemu maalumu ya kufanyia mazoezi, bwawa na kila kifaa kinachopatikana kwenye timu.
Kwetu sisi hiyo ni ngumu kuwa hivyo ni wachache sana ambao wanajitambua utakuta wana baadhi ya vitu ambavyo vinawafanya wawe katika ubora.
Yapo aina ya mazoezi ya kufanya kwa wakati huu sio yale magumu sana lakini ni muhimu kuyafanya kwa kuwa vifaa ni hafifu inakuwa ngumu kutimiza zile baadhi ya program kwa ufasaha.
Tuzidi kuchukua tahadhari na kundelea kuomba dua kwa kuwa hali bado sio poa na Serikali inazidi kuongeza nguvu katika kupambana na suala hili hivyo nasi tunapaswa tuunge mkono juhudi za Serikali bila kupinga.



UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa mpango mkubwa uliopo kwa sasa ni kujenga kikosi imara kwa ajili ya mashindano ya kitaifa na kimataifa kwa msimu ujao wa 2020/21.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa bado kuna mipango inaendelea kupangwa na mingine inatimizwa taratibu kufikia malengo.

"Kufika malengo yalipo sio safari ya siku moja kuna mchakato ambao tunapitia kwa hatua ambayo tupo ni lazima tuwe na subira pamoja na hesabu kali kufikia mafanikio kitaifa na kimataifa kikubwa ni sapoti pamoja na dua," amesema.

Azam FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Arstica Cioaba raia wa Romania na kapten wao akiwa ni Agrey Morris ipo nafasi ya pili Kwenye msimamo na kibindoni ina pointi 54 baada ya kucheza mechi 28


SHIRIKISHO la Soka la Kenya, (KKF) limesema kuwa hakuna matumaini ya kuendelea na ligi kwa hivi karibuni na matokeo yake, Gor  Mmahia wametajwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL)

Ligi Kuu ya Kenya ilisitishwa tangu mwezi March kutokana na janga la Covid-19 bila tarehe rasmi ya kurudi. Hadi wakati huo, Gor Mahia walikuwa wakiongoza msimamo kwa alama 54 baada ya kucheza mechi 23.

Siku ya Jumatano, Shirikisho la Soka la Afrika, (Caf), liliandika barua kwa Mashirikisho ya soka kufafanua njia itakayo tumika kumaliza msimu.

Rais wa FKF Nick Mwendwa ameweka wazi:-"Unawezaje kumaliza mechi 10 au 11 zilizobaki wakati hatutaweza kucheza ndani ya mwezi Mei na Juni,"

"Wachezaji wamekuwa nyumbani na wanapaswa kuanza mazoezi, kwa hivyo unapataje wikendi za kutosha kucheza mechi? Gor Mahia watapewa taji, tutapeleka jina lao kwa CAF ifikapo Ijumaa. Hakuna mjadala juu ya maswala haya."

Mwenda pia amethibitisha kupanda daraja kwa Nairobi City Stars. "Nairobi City Stars na timu iliyoshika nafasi ya pili (Bidco United),zote zimepanda daraja."

"Tulianza msimu na sheria, na ni sheria tunazotumia kama FKF. Ni wazi asilimia 68 ya mechi zimechezwa.

Kama kawaida, timu iliyowekwa katika nafasi ya tatu kwenye ligi daraja la pili itacheza mechi mbili-mbili ili kuamua ni nani anacheza kwenye KPL msimu ujao. .Tutakuwa na mechi za playoff" amesema.

 (Source: Goal]

DAVID Molinga, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa anataka kufunga mabao mengi zaidi pale Ligi Kuu Bara itakaporudi.

Molinga ametupia mabao nane ndani ya ligi akiwa ni kinara kwa Yanga ambayo imefunga mabao 31 kwenye mechi 27.

Molinga amesema:"Ikiwa nitapata nafasi zaidi ya kuanza kikosi cha kwanza pale ligi ikirudi nina amini nitafunga mabao mengi zaidi ya haya nane niliyonayo kwa sasa na yote yatawezekana kwani ninafanya mazoezi ," .

Ligi Kuu Tanzania Bara ilisimamishwa Machi 17 na Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kupatikana mgonjwa wa kwanza nchini


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa miongoni mwa washambuliaji walio hatari ndani ya Ligi Kuu Bara ni pamoja na Meddie Kagere.

Akizungumza na Saleh Jembe, Hitimana amesema kuwa amekuwa akiwatazama washambuliaji wengi uwanjani ambao ni hatari ambapo na Kagere ni miongoni mwao.

"Nimekuwa nikitazama washambuliaji wengi ambao ni hatari ndani ya ligi jina la Kagere ni miongioni mwao.

"Amekuwa na mwendelezo mzuri na wastani wa kufunga mabao ndani ya mechi ambazo anacheza ambapo ukitazama kwa sasa ana mabao zaidi ya 10 si wa kubeza," amesema.

Kagere amehusika kwenye jumla ya mabao 19 yaliyofungwa na Simba msimu huu ambayo imefunga mabao 63


DECLAN Rice nyota wa West Ham ameingia kwenye anga za Manchester United pamoja  na Chelsea ambazo zinawania saini yake.

West Ham mwanzoni mwa msimu huu walisema kuwa hawana hesabu za kumuuza kiungo huyo.

Kwa sasa presha inaonekana imekuwa kubwa kutokana na timu nyingi kuyumba kiuchumi hivyo uwezekano wa kuuzwa ni mkubwa.

Timu nyingi duniani zimeyumba kiuchumi kutokana na janga la Virusi vya Corona

RAIS wa Klabu ya Real Madrid, Florentino Perez ana ndoto ya kupata saini ya mshambuliaji wa PSG, Neymar Jr.

Neymar Jr kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa kusepa ndani ya PSG ambapo ilielezwa kuwa Barcelona nao walikuwa wanahitaji kumrejesha kwenye timu yake ya zamani.

Madrid iliyo chini ya Kocha Mkuu, Zinadine Zidane Inaamini kuwa Ikimpata mshambuliaji huyo Itaongeza nguvu ndani ya kikosi chake.

Msimu wa 2013-17 Neymar alikipa ndani ya Barcelona ambapo alicheza jumla ya mechi 123 na alitupia mabao 68 huku ndani ya PSG akiwa amecheza mechi 52 ametupia mabao 47


BEKI wa kimataifa Moussa Wague mali ya FC Barcelona ambaye anakipiga kwa Mkopo Nice, ametoa tani 12 ya vyakula kusaidia jamii yao katika eneo la Bignona nchini Senegal.

Wague amesema sababu za kufanya hivyo ni kuendelea kutoa sapoti na kusaidia vita dhidi ya Virusi vya Corona.

Katika eneo hilo hadi sasa hakuna hata kisa kimoja cha Covid 19 kilicho ripotiwa lakini yeye anaamini ni vizuri kwa wakazi wa eneo hilo kuanza kujiandaa na kuchukua tahadhari.


Beki huyo anayekipiga pia timu nyake ya Taifa ya Senegal ndani ya Klabu ya Nice amecheza mechi tano huku kwenye timu ya Taifa ya Senegal ya wakubwa akiwa amecheza jumla ya mechi 18 na ametupia bao moja

son amesema kuwa anafurahia maisha yake ndani ya klabu hiyo kutokana na sapoti anayopewa kutoka kwa mashabiki, wachezaji na uongozi kiujumla.

Morrison amekuwa kwenye ubora wake ambapo mchezo wake wa kwanza mbele ya Singida United alitoa pasi moja ya bao wakati Yanga ikishinda mabao 3-1.

"Tunaishi vizuri na kupeana sapoti kubwa kutoka kwa viongozi na wachezaji pia jambo ambalo linanifanya niwe na furaha kuwa hapa kwa sasa, maisha ni mazuri ila kikubwa kwa sasa ni muhimu kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona," amesema.

Morrison ametupia mabao matatu ndani ya Yanga Kwenye Ligi akiwa ametupia mabao matatu pia.

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa miongoni mwa vitu ambavyo unavikumbuka kwa sasa ni pamoja na ushindani wa Ligi Kuu Bara uliokuwa umeanza kushika kasi ila hawana la kufanya zaidi ya kuchukua tahadhari.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa na Serikali ili kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia kwa sasa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa ni ngumu kusahau ile kasi ya ligi ilivyokuwa lakini hakuna chaguo.

"Ilikuwa ni kasi nzuri ambayo ilikuwa imeanza kushika lakini kutokana na janga hili la Virusi vya Corona hakuna namna ni lazima tukubali kufuata utaratibu.

"Kila mmoja anakumbuka namna ushindani ulivyokuwa mkubwa lakini ninapenda kusema kuwa kwa sasa wote tunapaswa tuwe ni kitu kimoja kupambana na Virusi vya Corona," amesema.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 33 kibindoni ina pointi 33.


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroec amesema kuwa hana tatizo na kiungo wake mshambuliaji Ibrahim Ajibu na anaamini anaweza kuwa bora baadaye ikiwa ataongeza juhudi kwenye mazoezi.

Ajibu ni ingizo jipya msimu huu ndani ya Simba alijiunga nayo kwenye usajili wa dirisha kubwa akitokea Klabu ya Yanga ambayo alicheza misimu miwili akitokea Simba.

Sven amesema:-"Ni mchezaji mzuri na anauwezo mkubwa kwani kuna mechi nilikuwa ninampa nafasi na alikuwa anatimiza majukumu yake vizuri sina tatizo naye kabisa.

"Kikubwa nimekuwa nikimwambia afanye mazoezi kwa juhudi ili kuzidi kuwa bora," amesema.

Ajibu amefunga bao moja ndani ya Simba na kutoa pasi nne za mabao akitumia mguu wake wa kulia huku Simba ikiwa imefunga mabao 63.

ndani ya Juventus ameombwa na mabosi hao kutotimka kwenye kikosi hicho na adumu mpaka pale mkataba wake utakapomeguka.

Ronaldo mkataba wake ndani ya Juventus unatarajiwa kumeguka 2022 na kwa sasa anatajwa kuwindwa na Real Madrid pamoja na Manchester United ambao wanataka kumrudisha kikosini nyota wao wa zamani.

Kwa sasa Ligi Kuu ya nchini Italia haijaanza na bado Ronaldo hajarejea yupo zake Ureno ambapo alikwenda kumpumzika kutokana na Ligi kusimamishwa baada ya kuibuka janga la Virusi vya Corona.

Juventus ipo nafasi ya kwanza Serie A ikiwa na pointi 63 kibindoni baada ya kucheza mechi 26, imefunga mabao 50 huku Ronaldo akiwa ametupia mabao 21



BEKI chipukizi anayekipiga ndani ya Klabu ya Coastal Union ya Tanga, Bakari Mwamnyeto amesema kuwa anachotazama kabla ya kumwaga saini ndani ya timu ni maslahi pamoja na nafasi yake ya kucheza.

Nyota huyo inaelezwa anawindwa na Yanga pamoja na Simba ambazo zinahitaji saini yake kwa ajili ya msimu ujao.

Beki huyo amesema hana hiyana kukipiga kwenye Klabu hizo kwani uwezo anao.

 "Kwangu mimi sina hiyana ya kucheza Simba ama Yanga ila kikubwa ambacho ninakitazama ni maslahi binafsi na nafasi yangu ya kucheza kikosi ncha kwanza," amesema.

Inaelezwa kuwa dau la kumpata beki huyo chipukizi ni milioni 100 jambo linalowapasua vigogo hao kuziangusha mezani


KLABU ya Paris St Germain,(PSG) inaelezwa kuwa imetuma ofa kwa Manchester United ili kupata saini ya kiungo mshambuliaji Paul Pogba.

Pogba mwenye miaka 27 amekuwa akihusishwa kujiunga na PSG pamoja na Real Madrid ambazo zinahitaji saini yake.

PSG wameunganisha na ofa ya kiungo wao mwenye miaka 32 Angel di Maria ambaye aliwahi kusajiliwa na Manchester United.


SOGNE Yacouba, mshambuliaji anayekipiga ndani ya Asante Kotoko anatajwa kuingia anga za Simba na Azam.

Yacouba mwenye miaka 28 inaelezwa kuwa mkataba wake unameguka msimu huu hivyo atasaini akiwa mchezaji huru.

Mshambuliaji huyo inaelezwa kuwa anawatambua vema Simba kwani aliwahi kuwatungua kwenye moja ya mchezo wa Simba day Uwanja wa Taifa na ngoma ilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Mbali na Simba inaelezwa kuwa Free State ya Ghana inahitaji saini ya nyota huyo raia wa Burkina Faso


DARUESH Saliboko, mshambuliaji wa Lipuli amesema kuwa Pascal Wawa ni miongoni mwa mabeki wagumu kupitika kutokana na nguvu, akili pamoja na mbinu zake.

Wawa anakipiga ndani ya Klabu ya Simba iliyo nchini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji.

Akizungumza na Saleh Jembe, Saliboko amesema kuwa kazi kubwa ya mshambuliaji ni kupenya kwenye ngome za mabeki ili kufunga ila alikuwa anapata wakati mgumu mbele ya Wawa.

"Unapomkabili Wawa ni lazima ujipange katika kasi na kuruka juu, ana mbinu nyingi ambazo ukienda kichwakichwa unaweza kukata tamaa.

"Namshukuru Mungu sina hofu katika kupambana ila ninatanguliza nidhamu kila wakati kwani mchezo wa mpira unahitaji akili na utulivu," amesema.

Saliboko ni miongoni mwa wazawa wanaofanya vizuri ametupia mabao nane ndani ya Lipuli msimu huu

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.