KIUNGO wa zamani wa Yanga, Ally Yusuf maarufu kama Tigana amefariki jana hospitali ya Amana, iliyopo Ilala, Dar imeelezwa kuwa chanzo cha kifo chake ni ugonjwa wa tumbo la Kuhara.

Tigana alikuwa mchezaji wa zamani wa Yanga alikitumikia kikosi hicho vipindi viwili tofauti kwa mwaka 1994-1995 na baadaye mwaka 2001-2004 ambapo uongozi wa Yanga umesema kuwa umepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.

Amefariki akiwa na umri wa miaka 49 alizaliwa mitaa ya Ilala maeneo ya Saadani na kusoma shule ya msingi Uhuru mchanganyiko.

Miongoni mwa timu ambazo aliwahi kucheza enzi za uhai wake ni pamoja na Shaurimoyo Kids, Manyema Rangers, Simba, Pan Africans, Cadtes ya Mauritius na Twiga SC aliitwa Tigana kutokana na kufananishwa na kiungo wa Ufaransa miaka ya 1980 Jean Pierre Tigana.


Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema Peponi.
Amina

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.