JUMA
Mwambusi aliyekuwa kocha mkuu wa Mbeya City amesema kuwa hakuwa na chaguo la
kufanya ndani ya kikosi hicho zaidi ya kuachia ngazi ya kukinoa kikosi hicho
ili kuokoa jahazi lisizame.
Mwambusi
aliachia ngazi ndani ya klabu hiyo mwezi Novemba kutokana na timu kuwa na
mwenendo mbovu jambo ambalo lilikuwa linamkosesha raha.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Mwambusi amesema kuwa anamshukuru Mungu kila kitu
kinakwenda sawa ana amini Mbeya City itarejea kwenye ubora wake.
“Nimekuwa na
vijana kwa muda mrefu wakati mwingine unashindwa kuelewa tatizo lipo wapi kwa
kuwa vijana wanajituma wanatengeneza nafasi ila wanashindwa kufunga hivyo
tatizo hilo lilinifanya nami nisiwe na chaguo la kufanya,” amesema Mwambusi.
Post a Comment