Kuelekea kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili, wikiendi hii mabosi wa Yanga watakuwepo nchini Rwanda wakimuangalia kwa jicho la pili kiungo fundi Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ ambaye wanafikiria kumrejesha kikosini mwezi huu.

Yanga ipo katika mipango ya kuboresha sehemu mbili ambazo ni ushambuliaji na kiungo mchezeshaji katika usajili wa dirisha dogo utakaofunguliwa Desemba 16, mwaka huu na tayari mapendekezo yametolewa ya usajili huo.

Mtoa taarifa huyo alisema mabosi wawili kutoka Kamati ya Ufundi ya Yanga wikiendi hii watakuwepo nchini Rwanda kwa ajili ya kumuangalia Niyonzima atakayekuwa uwanjani akicheza mchezo wao wa ligi kuu akiwa na timu yake ya AS Kigali.

Aliongeza kuwa lengo la kwenda kumuangalia kiungo huyo ni kwa ajili ya kujiridhisha uwezo wake ule aliokuwa nao bado anao na wakiridhishwa naye haraka watampa mkataba ili ajiunge na timu hiyo kabla ya kukutana na watani wao Januari 4, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Niyonzima ambaye aliwahi kuichezea Simba msimu uliopita, miaka kadhaa nyuma aliwahi pia kuitumikia Yanga ambayo ilimfanya atambulike zaidi katika ramani ya soka.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.