DUNCAN
Ferguson amechukua mikoba ya Marco Silva ambaye amepigwa chini ndani ya
kikosi cha Everton kinachoshiriki Ligi Kuu England.
Silva
amedumu kwa muda wa miezi 18 amemaliza muda wake kwa misukosuko kibao
kwani mchezo wake wa mwisho alifungwa mabao 5-2 na Liverpool.
Silva
amekuwa kocha wa nne kutimuliwa ndani ya kikosi hicho baada ya timu
hiyo kuwa chini ya bilionea Farhad Moshiri kuanzia Februari 2016 na
inaonekana kuwa hana mpango mkubwa na Ferguson.
Inatajwa kuwa David Moyes ambaye alikuwa kocha wa timu hiyo mwaka 2002-2013 anasubiriwa kujibu maombi ya kuionoa timu hiyo.
Ferguson
alikuwa anafanya kazi na Silva ambaye amepigwa chini, timu hiyo ipo
nafasi ya 18 baada ya kucheza mechi 15 ina pointi 14.
Post a Comment