JUMA Kaseja, mlinda mlango wa timu ya KMC si miongoni mwa wachezaji waliokwea pipa kuelekea Uganda na Kilimanjaro Stars kwa kile kilichoelezwa kuwa ni matatizo ya kiafya.

Awali Kaseja ambaye ni mlinda mlango mkongwe aliyeipeleka Stars kwenye michuano ya Chan 2020 itakayofanyika nchini Cameroon aliitwa kwenye kikosi cha awali ambacho kilikuwa na magolikipa wanne ikiwa ni pamoja na Aishi Manula wa Simba, David Kisu wa Gormahia na Metacha Mnata wa Yanga.

Juma Mgunda, kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars amesema kuwa wachezaji walioachwa wana sababu maalumu ikiwa ni pamoja na yale yao binasi pamoja na yale ya kiafya.

Kilimanjaro Stars itamenyana na Kenya Desemba 8 nchini Uganda kwenye michuano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Chalenji).

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.