ARSENAL imeanza kuwa na hofu ya kumpata kocha wa Leicester City, Brendan Rodgers baada ya timu yake kugoma kumuachia.
Rodgers amekuwa na msimu mzuri ndani ya Ligi Kuu England na timu yake imekuwa ikionyesha kiwango cha juu Sana uwanjani.
Kwa sasa Leicester City ipo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 15 imejiwekea kibindoni jumla ya pointi 35.
Kocha huyo wa zamani wa Liverpool anatajwa kuwa anaweza kujiunga na Arsenal ambayo imempiga chini kocha wao Unai Emery aliyedumu klabuni hapo kwa muda wa miezi 18.
Imetajwa kuwa kumpata kocha huyo timu yoyote lazima ivunje benki na kuweka mezani kitita cha pauni milioni 14 zaidi ya bilioni 35 kutokana na hali hiyo kumekuwa na taarifa kuwa Freddie Ljungberg atabaki kwenye nafasi hiyo kwa muda mrefu.
Post a Comment