BAKARI Mwamyeto, beki anayefanya vema ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya Coastal Union amesema kuwa hana tatizo endapo atatakiwa kumwaga saini ndani ya klabu ya Yanga kwa sasa endapo watafuata utaratibu.
Mwamnyeto amekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga kwa sasa yupo nchini Uganda na timu ya taifa ambayo inashiriki mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Chalenji).
Akizungumza na Saleh Jembe, Mwamnyeto amesema kuwa anatambua umuhimu wa kazi yake anayoifanya hawezi kufanya makosa popote atakapokuwa kwani anajiamini.
"Unajua mimi ni mchezaji na kazi yangu ni kucheza, sina tatizo na Yanga iwapo watakuja mezani na kuhitaji saini yangu kikubwa ni kuona namna gani watafuata utaratibu," amesema.
Post a Comment