Mtanzania
Mbwana Samatta ameondoka katika kampuni ya uwakala ya First For Players
na kujiunga na Spocs Consultant inayomsimamia Mohamed Salah wa
Liverpool, Samatta anakuwa mchezaji wa pili mwenye thamani ya juu kwa
wanaosimamiwa na kampuni hiyo baada ya MOSalah.
Samatta ambaye ni mchezaji namba 2 kwa thamani katika
list ya wachezaji zaidi ya 100 wanaosimamiwa na Spocs Consultant,
aliingia mkataba na First For Players December 22 2018 lakini ameamua
kubadilisha wakala kwa sasa.
Samatta anayetajwa
kuwa na thamani ya pound milioni 12 kwa mujibu wa mtandao wa transfer
Market, anaamini kufanya huko na uzoefu wa kampuni hiyo mpya kunaweza
kusaidia ndoto yake ya kucheza EPL.
Post a Comment