Usiku
wa December 2019 nchini Ufaransa katika jiji la Paris zilifanyika tuzo
za Ballon d’Or 2019, huku wengi wakitaka kujua ni nani atakuwa mshindi
kati ya Van Dijk, Ronaldo na Lionel Messi.Lionel Messi ashinda tuzo ya 6
ya Ballon d’Or na kumuacha Ronaldo
Lionel Messi wa FC Barcelona ndio mshindi wa tuzo ya
Ballon d’Or 2019, hiyo ikiwa ni tuzo yake ya 6 ya Ballon d’Or akimzidi
mpinzani wake wa muda wote Cristiano Ronaldo aliyewahi kutwaa tuzo hiyo
mara 5.
Wengine
waliofanikiwa kushinda tuzo katika usiku wa Ballon d’Or 2019 ni beki wa
Juventus Matthijs De Light tuzo ya mchezaji bora kijana (Kopa Trophy)
kwa kuwashinda Jadon na Joao.
Golikipa wa
Liverpool Alisson Becker akiwa ndio mshindi wa tuzo ya kipa bora wa
mwaka na Megan Rapinoe wa timu ya taifa ya wanawake ndio akashinda tuzo
ya mchezaji bora wa kike (Ballon d’Or).
Post a Comment