ZAMALEK imempiga chini jumla Kocha wao raia wa Serbia, Milutin Sredojevic 'Micho' kutokana na kuwa na matokeo mabovu ndani ya timu hiyo.
Presha ilikuwa kubwa baada ya Zamaleki kuchapwa mabao 2-1 na Enppi kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Misri wiki iliyopita na kuifanya timu hiyo kuwa nafasi ya tano kwenye Msimamo.
Kichapo cha mabao 3-0 mbele ya TP Mazembe siku tano nyuma kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye mchezo wa Kwanza wa ufunguzi wa kundi A kulifungua njia yake ya kupigwa chini .
Micho amesimamia timu hiyo kwenye mechi 12 ameshinda mechi saba akipoteza mechi nne na sare moja pekee.
Post a Comment