MBWANA Samatta nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ambaye anakipiga kwenye timu ya Genk huko nchini Ubelgiji jina lake limetajwa kwa wale wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kitu cha kujivunia na kinapaswa kiwape hasira wachezaji wetu wengine.
Tunamuona Samatta
namna anavybadilika na kukubali kujifunza kila saa kila wakati akiwa na
timu yake ya Genk na hata akiwa na timu ya taifa kitu ambacho wachezaji
wetu wengi wa ndani wanakikosa kwa kujisahau na kufikiri kwamba kucheza
timu ambazo wanazipenda kutawapa mafanikio ya jumla hapana kuna mambo
yamebadilika.
Samatta ni mchezaji
wa kawaida kwa level zetu lakini ule ukawaida wake ameweza kuutumia kwa
umakini jambo ambalo wengi wanashindwa kufanya hasa kwa wakati huu ambao
teknolojia inazidi kukua na soka likizidi kutazamwa na wengi
wanashindwa kufanya.
Kutajwa kwake na
kushindanishwa na wachezaji wenye majina makubwa ikiwa ni pamoja na
Mohamed Salah, Sadio Mane wote wanaokipiga ndani ya Liverpool kwenye
Ligi Kuu ya England sio hatua ya kubeza.
Mchezaji Mane leo
anakula sahani moja na Samatta ni kitu kikubwa na kinachofikirisha
kwamba kutoa wachezaji wengi nje kuna manufaa na matunda yake ni haya
ambayyo tunaanza kuyaona.
Samatta amefungua
njia wachezaji wengine mna jambo la kujifunza kutoka kwake ili kuongeza
idadi ya ushindani ndani ya kuwania tuzo kubwa zikitokea tena wakati
mwingine.
Tunaona kwamba
Liverpool wao wametoa wachezaji wawili ambao ni Mane na Salah basi ifike
wakati wachezaji ambao watachaguliwa wanaokipiga nje iwe wachezaji
watatu kutoka Tanzania.
Inawezekana endepo
wachezaji wetu wataamua kujituma na kufanya kazi kwa juhudi bila
kuangalia nani anasema nini ama wakacheze timu gani hakuna anayefanikiwa
kwa kuchagua aina ya maisha.
Kwa hili ambalo
limemtokea Samatta hata akishindwa kubeba tuzo sio mbaya japo ni maombi
yetu atwae kabisa na hiyo tuzo aipeleke Mbagala ambako ndipo maskani
yake ilipo.
Ikitokea ameshindwa
ni suala la kukubalina na matokeo kisha kujipanga upya kwa wakati
mwingine kwani kushindwa ni sehemu ya matokeo kwenye soka.
Pia tumeona kwa
wchezaji wa ndani ambao wanawania tuzo hiyo yumo Meddie Kagere
anayekipiga Simba ambaye ni raia wa Rwanda na Emmanuel Okwi ambaye kwa
sasa anakipiga Ittihad yeye ni raia wa Uganda.
Okwi aliwahi kucheza
ndani ya Simba msimu uliopita kwa sasa ameondoka ndani ya Simba
anaendelea na maisha yake nje ya Simba lakini anafuatiliwa na ametajwa
kwenye tuzo hii.
Hapa kuna kitu cha
kujifunza kwa timu zetu namna zinavyofanya usajili kwa kuangalia aina
gani za wachezaji wanapaswa waendelee kuwepo ndani ya timu ama kuachana
nao.
Haina maana kwamba
nawasema mabosi wao kwamba walikosea kumuacha hapana kuna wakati ni
lazima ukubali kwamba hata kama mchezaji anahitaji dau kubwa kiasi gani
na ni muhimu haina namna ni lazima uvunje tu benki.
Yote kwa yote
kutajwa kwa hawa wote wa kigeni kuna jambo la kujiuliza kwa wachezaji
wetu wa Bongo kwani wao wanacheza ligi ya wapi?
Muda wao wa
kupambana ili wakati ujao wawe miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo
kwa wachezaji wa ndani na sio kujivunia eti mchezaji aliwahi kucheza
Simba ama Yanga sio sawa.
Ikumbukwe kuwa
wakati timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inafungwa na Libya lawama
nyingi zilielekezwa kwa Samatta kutoka kwa mashabiki.
Wapo sahihi kwa kile
ambacho wanakisema kwa kuwa wanamfuatilia na kumpenda mchezaji wao
hivyo wanaona kuna kitu ambacho kinakosekana kwakwe akiwa na timu ya
taifa.
Kwa kuwa maoni ya
wadau yalimfikia Samattta mwenyewe alikiri kulipokea na kukubali
kuyafanyia kazi maoni aliyoyayapokea na aliweka wazi kwamba wadau
hawajaridhishwa na kile alichokifanya.
Kwa lugha ya mtaani
tunasema alikubali kupokea ujumbe kwamba alizingua kwenye timu ya taifa
hakukasirika aliweka wazi kwamba ameyapokea maoni na atayafanyia kazi.
Inaonyesha namna gani yupo tofauti na wengine, nakumbuka kuna mchezaji mmoja aliwahi kuambiwa kwamba amechuja akawa mkali.
Lugha yake
aliyotumia kuwajibu mashabiki haikuwa ya kiungwana alidai kwamba
anaonewa kumbe alisahau kwamba mpira ni mchezo wa wazi na mwisho wa siku
tulishuhudia anguko lake.
Kinachotakiwa
kufanyika kwa wachezaji wetu wa Bongo ni kujifunza na kufuata kile
ambacho wanashauriwa kwani anayekushauri leo kwamba umefeli ina maana
kwamba anakufuatilia kwa muda mrefu.
Hawezi kukurupuka
kutoka kusikojulikana na kudai kwamba umezingua ilihali hakujui wachache
sana huwa wanafanya hivi lakini bado kuna umuhimu wa kuchukua maoni yao
na kuyafanyia kazi.
Kwa yule ambaye
hapendi kukosolewa ni rahisi kwake kupata anguko kwani ataamini kwamba
yeye anajua kila kitu jambo ambalo halina ukweli katika maisha.
Maisha ya soka yana
kupanda na kushuka katika haya yote mashabiki ni washauri wao jambo
ambalo litawafanya wazidi kuwa bora katika kile ambacho wanakifanya siku
zote bila kukoma.
Endapo Samatta
angepuuza yale ambayo mashabiki wake wanamwambia huenda angeshindwa
kujua wanahitaji nini na kitu gani ambacho anakosea kwa sasa hasa kwa
mashabiki.
Ukweli ni kwamba
kuna wakati mpira humkataa mchezaji kutokana na siku kuwa tofauti ila
kinachotakiwa kwa mchezaji ni kupambana kwa ajili ya mafanikio yake na
timu kiujumla.
Tunaona kwamba Stars
imeshindwa kupata matokeo mbele ya Libya hii isiwaumize jumla mashabiki
na kuamua kujiweka pembeni bado safari ipo na kazi inaendelea.
Wahenga walisema
kuwa kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi kwa hatua ya kwanza kazi
haijaisha bado inaendelea na mechi zipo mkononi mwa Stars kufuzu ni
suala la muda tu.
Post a Comment