MEDDIE Kagere, mshambuliaji tegemeo wa Simba amesema kuwa kinachombeba kufanya vizuri ni maombi kwa Mungu pamoja na juhudi ndani ya Uwanja.

Kagere amehusika kwenye jumla ya mabao 16 ndani ya Simba yenye mabao 38, akifunga mabao 12 na kutoa pasi za mabao nne msimu huu 2019/20.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 44 ikiwa imecheza jumla ya mechi 17, watani zao Yanga wapo nafasi ya nne na pointi zao 28 kwenye mechi 15 walizocheza wakiachwa kwa jumla ya pointi 16.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kagere amesema kuwa anafurahi kuona timu yake inashinda na ushindani ambao wanaupitia unawapa nguvu ya kuendelea kupambana na kinachombeba ni juhudi.

"Mungu katika kila ninachokifanya, juhudi ya kufanya mazoezi na kufanyia kazi yale ninayofundishwa kikubwa tunachohitaji ni matokeo, mengine baadaye," amesema.

Simba leo itakuwa kazini Uwanja wa Uhuru ikimenyana na Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.