JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union amesema kuwa leo watatumia mbinu mpya kuimaliza Simba Uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mgunda amesema kuwa wanaitambua vema Simba mbinu zao watapambana kupata pointi tatu muhimu.

"Tunawatambua wapinzani wetu na namna ambavyo wanafanya tunajua, tupo tayari kupata pointi tatu mashabiki watupe sapoti na mbinu zetu ni kali na mpya," amesema.

Coastal Union ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 30 na Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 44 zote zimecheza mechi 17.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.