LEO Uwanja wa Uhuru kutakuwa na mchezo wa ligi kuu kati ya Simba na Coastal Union ambao unatarajiwa kuwa ni wa kukata na shoka kwa timu zote mbili kutokana na vita ya kuwania ubingwa inayoendelea.

Simba ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 44 baada ya kucheza mechi 17 itakutana na Coastal Union iliyo nafasi ya  tatu na pointi zake 30 baada ya kucheza mechi 17.

Rekodi zinaonyesha kuwa kwa msimu uliopita wa 2018/19 ambao Coastal Union ilipanda daraja iliambulia kichapo mechi zake zote mbele ya Simba jambo litakaloongeza ugumu kwa timu zote.

Mchezo uliochezwa Dar, Uwanja wa Uhuru, Simba ilishinda mabao 8-1 na ule uliochezwa Tanga, Mkwakwani Simba ilishinda mabao 2-1.

Jumla Coastal Union ilifungwa mabao 10-2 na kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, wachezaji wawili walifunga hat trick kutoka Simba ambao ni Emanuel Okwi na Meddie Kagere.

Sven alisema kuwa anahitaji kuona wachezaji wakipambana kupata pointi tatu, huku Juma Mgunda wa Coastal Union akisema kuwa hana mashaka na uwezo wa wachezaji dakika tisini zitaongea.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.