KOCHA wa zamani wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino anatamani kuona siku moja anarejea katika klabu ya Newell's Old Boys akiwa na staa wa Barceona Lionel Messi.
Pochettino ambaye ni raia wa Argentina aliwahi kuichezea klabu hiyo wakati anaanza soka kama ambavyo Messi naye ameanzia soka katika klabu hiyo.
“Matumaini yangu ni kuona siku moja narejea katika klabu ya Newell's Old Boys naona kama nachelewa lakini itakuwa ndani ya miaka 10 ijayo, ila nitakuwa na Messi.
Pochettino alisema kuwa matumaini yake makubwa yako hivyo lakini anaamini kuwa Messi atacheza hata Kombe la Dunia lijalo.
“Messi atacheza Kombe la Dunia Qatar 2022 na atafanya vizuri bila kujali umri wake atapambana tu, unajua uwepo wake ndani ya timu ni kitu kikubwa sana ataipambania tu Argentina kwenye michuano hiyo," amesema.
Post a Comment