SHIJA Richard, Mjume wa Kamati ya Yanga inaelezwa kuwa amejiuzulu nafasi hiyo leo Machi 27 bila kuweka wazi sababu za kujiuzulu kwake.


Richard ni miongoni mwa wajumbe watatu wanaotuhumiwa kutokuwa na mahusiano mazuri na Kampuni ya GSM ambayo hivi karibuni ilitangaza kubakia kuwa mdhamini kama mkataba wake unavyoelekeza.

 Richard amedai kuwa klabu hiyo ni kubwa kuliko mtu hivyo ameamua kujiweka pembeni. 


"Nimeamua kwa hiari yangu kujiuzulu nafasi zote za uongozi katika klabu yangu ya Yanga ambayo ni kubwa kuliko mimi na kuliko mtu yeyote.

 "Ukweli hata usipousema, huwa una tabia ya kujitokeza wenyewe japo taratibu lakini huwa unadumu milele," imeeleza taarifa hiyo.

Mjumbe mwingine ambaye amejieungua ni pamoja na Rodgers Gumbo ambaye naye inaelezwa kuwa amejiengua.

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli ili azungumzie suala hili hakuwa tayari.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.