MANUEL Neuer, mlinda mlango wa Bayern Munich ameingia kwenye anga za Klabu ya Chelsea ambayo inaiwinda saini yake.
Frank Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea anahitaji kupata mlinda mlango mpya ndani ya kikosi hicho na hali hiyo itategemea iwapo watamuuza  kipa wao Kepa Arrizabalaga.
Kepa amekuwa na balaa la kutengwa ndani ya msimu huu kutokana na kile kinachoelezwa kuwa kiwango chake kumeshuka.
Mlinda mlango huyo machachari langoni katika kuokoa michomo ya hatari hakuwa chaguo la Lampard kwenye mechi nne zilizopita za Februari ndani ya Ligi Kuu England.
Neuer mkataba wake unameguka mwaka 2021 ndani ya Bayern Munich ila unampa nafasi ya kufanya mazungumzo na klabu nyingine iwapo inataka kumpa dili jipya.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.