SAID Makapu, beki wa Yanga amesema kuwa kinachompa namba kwa sasa ndani ya kikosi cha Yanga ni kuaminiwa na Kocha Mkuu, Luc Eymael tofauti za zama zilizopita alipokuwa Kocha Mkuu Mwinyi Zahera.
Makapu amekuwa kwenye ubora wake msimu huu akiwa chini ya Eymael ambapo kwenye dabi walipokutana na Simba aliwadhibiti washambuliaji wa Simba Meddie Kagere na John Bocco kwa umakini ilikuwa Machi 8 na Yanga ilishinda kwa bao 1-0.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.
"Nimekuwa bora kutokana na kuaminiwa na Kocha Mkuu wa sasa Eymael, Zahera alikuwa haniamini ndio maana hakunipa nafasi ndani ya kikosi cha kwanza.
"Nina amini kwamba wakati ujao nitazidi kuwa bora kwani tunashirikiana vema na wachezaji wenzangu jambo ambalo linanifanya nifurahie maisha ndani ya Yanga,".

Post a Comment