MECKY Maxime Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa alipewa mkataba wa kujiunga na Yanga, lakini kutokana na kutoļ¬kia baadhi ya makubaliano, alishindwa kuusaini na mpaka leo bado anao.
Maxime aliwahi kuifundisha Mtibwa Sugar, amesema alipewa mkataba huo Desemba mwaka jana kipindi ambacho Yanga ilikuwa ikinolewa na kocha wa muda, Charles Mkwasa akisaidiwa na Said Maulid ‘SMG’.
“Ni kweli nina mkataba wa Yanga ambao walinipa tangu mwishoni mwa mwaka jana, lakini sijausaini kutokana na baadhi ya mambo kutokwenda sawa.
"Mimi bado ni mwajiriwa wa Kagera Sugar na mambo yakienda kama inavyotakiwa sina hiyana kujiunga na Yanga,” amesema Maxime.
Kagera Sugar kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu huu uliochezwa Uwanja wa Uhuru iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Mchezo huo ulikuwa ni wa kwanza kwa Kocha Mkuu, Luc Eymael alipotua kuchukua mikoba ya Mwinyi Zahera.
Post a Comment