ABDULAZIZ Makame kiungo wa Yanga inaelezwa kuwa amekana kwamba yeye sio mchezaji wa Yanga bali ni wa Majimaji kutokana na sauti inayosambaa kwenye mitandao ya jamii kuenea akisikia akiongea hayo.
Kwenye sauti hiyo inayosadikiwa kuwa ni ya Makame inaeleza kuwa chanzo kikubwa cha kukana kuwa yeye sio mchezaji wa Yanga ni kutohusishwa kwenye mgawo wa fedha za GSM ambao ni wadhamini wa Yanga kwa sasa.
Sauti hiyo imesikiaka ikizungumza namna hii:-"Kwa Mimi, Mimi Makame, kama watu wengine hawana namba zangu mimi Makame umenifahamu eh, simuogopi mtu, simuhofii mtu kama GSM ametoa hela zake gawaneni nyie kwa sasa sisi wengine ni wachezaji wa Majimaji.
"Sisi kukaa nyumbani tunaonekana kama tumependa umenifahamu, hii ni mipango ya Mungu, sisi hatutaki muharibu hata mara moja nyoyo zetu tunataka mshinde na hilo wazo ulilotoa Molinga ni nzuri.
"Huyo GSM angekuwa asingewagawia hela namna hii, sie watu wa nyumbani, hizo hela zikipatikana msinigawie hata kidogo peaneni wenyewe watu wa Yanga," .
Alipotafutwa Makame ili azungumzie suala hilo kwa njia ya simu hakupokea simu.
Post a Comment