JOHN Bocco, nahodha wa Simba amempiku nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi kwa kutengeneza pasi nyingi za mabao na kucheka na nyavu ndani ya uwanja licha ya kucheza kwa muda mfupi.
Tshishimbi ambaye ni nahodha wa Yanga msimu huu amecheza mechi 23 kati ya 27 ambazo Yanga imecheza na ametumia dakika 1,936 kukiongoza kikosi cha Yanga huku Bocco wa Simba akicheza mechi 12 sawa na dakika 782 na ametumia dakika hizo kutokana na kuanza msimu akitibu majeraha.
Kwa dakika zake 782, Bocco amefunga mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara na kutoa pasi mbili za mabao akimpiku Tshishimbi aliyetumia dakika 1,936 akiwa na pasi moja ya bao aliyoitoa mbele ya Biashara United Uwanja wa Taifa wakati Yanga ikishinda bao 1-0 likifungwa na Tariq Seif.
Mechi alizocheza Bocco akiwa na kitambaa cha unahodha ni mbele ya Ndanda (90), Yanga, (22), Alliance (7), Namungo (12), Coastal Union, (81), Polisi Tanzania, (90), Mtibwa Sugar,(74), Kagera Sugar, (84), Biashara United,(90), Lipuli (90) Yanga (90) na Singida United (52).
Mechi za Tshishimbi ilikuwa mbele ya Ruvu Shooting (90), Mbao FC (90), JKT Tanzania (90), Mbeya City (90), KMC (90), Prisons (26), Biashara United (20), Ndanda (90), Alliance (90), Simba (90), Azam FC (90), Singida United (90), Mtibwa Sugar (90), Lipuli (90), Ruvu Shooting (90), Mbeya City (90), Prisons (90), Polisi Tanzania (90). Coastal Union (90), Mbao (90), Simba (90), KMC (90), Namungo (90).
Post a Comment