JONAS Mkude, kiungo mkabaji ndani ya klabu ya Simba amesema kuwa watu wengi wanaomsema vibaya hawezi kuwazuia kwa kuwa wameamua kumwandama bila kujua kinachomsumbua.

Mkude amesema kuwa kushindwa kwake kujiunga ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars hivi karibuni kumeibua maneno mengi kwa kila mmoja kutaja sababu anazozijua.

"Wengi wamesema vile ambavyo wanajua wao ila ukweli unabaki kwamba mimi ni binadamu na matatizo yananikuta pia, haina maana kwamba sipendi kutimiza majukumu yangu hapana kuna wakati mwingine nakwama kutokana na matatizo ambayo ninayapata," amesema.

Kambi ya Stars iliyokuwa inajiaandaa na michuano ya CHAN ilivunjwa hivi karibuni kwa ajili ya kuzuia maambukizi zaidi ya Corona, Mkude alichaguliwa kujiunga na kambi hiyo kabla ya kuvunjwa ila hakuripoti mpaka kambi ilipovunjwa.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.