MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kutokana na tamko la Bodi ya Ligi Kuu Bara kuwa endapo Ligi Kuu Bara itarejea timu zitacheza bila mashabiki hali hiyo haitapendeza kwani mashabiki wamekuwa wakinogesha mpapaso.

Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Machi 17 ilisimamisha shughuli zote zinazohusu mikusanyiko isiyo ya lazima ikiwa ni Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Wanawake zimesimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Bwire amesema ni jambo la msingi ambalo limefanywa na Bodi ya Ligi kuzuia mashabiki ili kupambana na Virusi vya Corona ila kuna mambo mengine hayatapendeza.

“Siku zote nimekuwa nikisema kwamba Ruvu Shooting inacheza kama Barcelona, sasa kutokana na kuzuiwa kwa mashabiki kujitokeza uwanjani iwapo ligi itaanza mpapaso hautapendeza sana lakini ni lazima tuzingatie utaratibu.

“Tunaomba hili lipite na ligi irejee kwani hili jambo siyo la kuchukulia utani Watanzania pia ni muhimu kuchukua tahadhari na Virusi vya Corona ili wawe salama,” amesema Bwire.

Ruvu Shooting ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo ikiwa na pointi 39 baada ya kucheza mechi 28 za Ligi Kuu Bara.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.