LIGI Kuu England ikiwa imesimama kwa muda kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona na inatarajiwa kurejea April 30 itategemea kutengamaa kwa hali.

Hawa hapa ni watupiaji ndani ya Ligi Kuu England:- Jamie Vardy ametupia mabao 19 anakipiga Leicester City ipo nafasi ya tatu na pointi 53 imefunga mabao 58.

Aubameyang anakipiga Arsenal ametupia mabao 17 timu yake ipo nafasi ya tisa ina pointi 40 imetupia mabao 40.

Sergio Aguero ametupia mabao 16 anakipiga Manchester City iliyo nafasi ya pili na pointi 57 imefunga mabao 68.

Mohamed Salah anakipiga Liverpool timu yake ipo nafasi ya Kwanza ina pointi 82 na imetupia mabao 66 akiwa amefunga mabao 16.

Danny Ings anakipiga Southampton ametupia mabao 15 Kati ya 35 timu yake ipo nafasi ya 14 na pointi 34.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.