UONGOZI wa Barcelona unampango wa kupitisha panga la mishahara kwa wachezaji wake ili kuongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.

Wachezaji wa Klabu ya Barcelona inaelezwa kuwa wapo katika mvutano na Bodi ya timu hiyo kufuatia pendekezo la Bodi kutaka kuwakata asilimia 70 ya mishahara wakati huu Ligi ikiwa imesimama kwa sababu ya Virusi vya Corona.

Baadhi ya wachezaji wameripotiwa kukubali huku wengine wakigoma kabisa kukatwa mishahara yao.


 Barcelona na Real Madrid wamekuwa wakipata mgawo mkubwa kwenye mapato ya siku za mechi, wapo katika wakati mgumu kutokana na kufutwa kwa mechi za Ligi Kuu ya Hispania – La Liga na haijulikani zitarudia lini.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.