IMEELEZWA kuwa nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi ameongeza kandarasi ya miaka miwili kuendelea kukipiga ndani ya klabu hiyo.
Kulikuwa na sarakasi za mkataba wa nyota huyo ambaye kandarasi yake imebaki miezi minne kumeguka.
Habari zinaeleza kuwa mtikisiko wa Simba kudaiwa kuwa wanaiwinda saini yake umewafanya mabosi wamuite mezani kumalizana naye.
"Yote mema licha ya tafrani hivi karibuni ndani ya kamati zetu tendaji, tumefanikiwa kumuongezea Tshishimbi kandarasi ya miaka miwili,mvutano ulikuwa mkubwa lakini mwisho wa siku kila kitu kimekwenda sawa," ilieleza taarifa hiyo.
Tshishimbi hivi karibuni alisema kuwa yupo kwenye mazungumzo na mabosi wa Yanga wakifikia muafaka atamalizana nao.
Post a Comment