JUSTIN Shonga, mshambuliaji anayekipiga ndani ya Klabu ya Orlando Pirates inaelezwa kuwa bado yupo kwenye vichwa vya mabosi wa Simba wanaotaka kuipata saini ya nyota huyo huku kinachoipasua kichwa ikiwa ni dau lililowekwa mezani.
Shonga ana umri wa miaka 23 alijiunga na Klabu ya Orlando Pirates akitokea Klabu ya Nkwazi FC ya Zambia mwaka 2017 kwa dau la milioni 383.
Nyota huyo raia wa Zambia ana nafasi pia ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia kwani tangu mwaka 2017 mpaka sasa tayari amecheza jumla ya mechi 24 ambazo ni sawa na dakika 2,160 na ametupia mabao 13 akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 166.
Habari zimeeleza kuwa mabosi wa Simba wanahaha kumpata,Shonga ambaye licha ya pesa inayohitajika kuanzia shilingi milioni 800, kuna uwezekano wa kupungua na kumnyakua mwamba huyo ndio maana mazungumzo yanaendelea.
Katibu Mkuu wa Simba, Dk Arnold Kashembe amesema kuwa masuala ya usajili yapo kwenye kamati ya usajili.
Post a Comment