SAID Ndemla kiungo wa Simba msimu wa 2019/20 ametumia dakika 270 sawa na mechi tatu uwanjani kwenye mechi za Ligi Kuu Bara wakati Simba ikiwa imecheza mechi 28 ambazo ni sawa na dakika 2,520.

Ndemla amekosekana kwenye mechi 25 ambazo ni sawa na dakika 2,250 uwanjani.

Mechi mbili alianza wakati wa utawala wa Patrick Aussems ambapo alicheza mbele ya Biashara United wakati Simba ilishinda mabao 2-0, Singida United wakati Simba ilishinda bao 1-0.


Kwenye utawala wa Sven Vandenbroeck amecheza mechi moja mbele ya Ndanda FC wakati Simba ilishinda mabao 2-0.

Simba imecheza mechi 28 ipo nafasi ya kwanza na pointi 71 imebakiza mechi 10 kukamilisha mzunguko wa kwanza.

Ligi Kwa sasa imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.