PATRICK Aussems, aliyekuwà Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kusambaa kwa Virusi vya Corona kumetibua mipango yake ya kutua Afrika Kusini kusaini dili lake jipya.
Aussems alipigwa chini na Simba msimu huu wa 2019/20 akiwa ameongoza mechi 10, akishinda nane, sare moja na kichapo kimoja.
Alikuwa na mpango wa kuibukia Afrika Kusini ambapo inaelezwa amepata timu ya kuifundisha ila Virusi vya Corona vimemfanya abaki nchini Ubelgiji.
"Nimepokea ofa nyingi na siku chache zilizopita nilikuwa Afrika kufanya mazungumzo na timu moja kubwa Ila siwezi kitaja ipo wapi na nchi gani Kwa kuwa hakuna kilichofanyika kutokana na Corona.
"Bado ni muhimu kutambua kwamba ili kuzungumza jambo ni azima liwe na uhakika na limekamilika ninaamini hali ikitulia mambo yataendelea kwani kwa sasa hakuna kinachofanyika,"amesema.
Post a Comment