HARUNA Niyonzima, Kiungo mshambuliaji wa Yanga amemshauri kiungo wa Simba Said Ndemla kutafuta changamoto mpya ili apate nafasi ya kucheza.
Ndemla kwa sasa ndani ya Simba iliyo chini ya Sven Vandenbroeck amekuwa hana nafasi ya kucheza kwani kwenye mechi 18 ambazo kocha huyo amesimamia amecheza mechi moja.
Mechi hiyo ilikuwa Uwanja wa Taifa ambapo Simba ilicheza na Ndanda FC na Simba ilishinda mabao 2-0.
Niyonzima amesema:"Ndemla ni kiungo mzuri na ana uwezo mkubwa wa kucheza tatizo ni kwamba anakosa namba kutokana na ushindani uliopo, wakati wake ni sasa wa kutafuta changamoto mpya ili alinde kipaji chake,".
Post a Comment