KLABU ya Chelsea inayonolewa na Kocha Mkuu Frank Lampard imevutiwa na uwezo wa nyota anayekipiga ndani ya Borrusia Dortmund, Jadon Sancho.
Hesabu za Lampard zinagogana na Kocha Mkuu wa Manchester United Ole Gunnars Solskajer ambaye naye pia anapendezwa na uwezo wa nyota huyo Sancho.
Timu zote kwa sasa mpango wao ni kuona namna gani zitapata saini ya Sancho lakini inaelezwa kuwa dau linaweza kuwa tatizo kwa sasa kutokana na klabu nyingi kupitia kwenye wakati mgumu kiuchumi kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona. 
Sancho amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ambapo ndani ya Bundesliga timu yake ikiwa imecheza mechi 23 ametupia mabao 14 na kutoa pasi 15 za mabao.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.