BERNARD Morrison Kiungo Mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kikubwa anachokifanya kwa sasa akiwa nyumbani ni kufanya mazoezi binafsi ili kulinda kipaji chake.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Serikali kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ilitoa tamko hilo Machi 17.

Morrison amesema kuwa kwa mchezaji ni jambo la msingi kulinda kipaji chake ili awe bora.

"Mchezaji ni lazima kulinda kipaji chake ili awe bora kwani kwa sasa ligi ikiwa imesimama na mchezaji akipumzika itakuwa hatari kwake kwa upande wa kiwango chake, hivyo muhimu ni kufanya mazoezi," amesema.

Morrison amefunga mabao matatu ndani ya Yanga kati ya mabao 31 ambayo yamefungwa kwa msimu huu wa 2019/20. 

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.