SIMBA wana nafasi kubwa ya kumpata mshambuliaji huyo anayekipiga ndani ya Klabu ya Orlando Pirates Justin Shonga iwapo wataweka pesa ya kutosha kutokana na kocha wa sasa wa timu hiyo kutomkubali.
Spoti Xtra limezungumza na Ofisa Habari wa Orlando, Thandi Merafe kwa njia ya simu moja kwa moja kutoka Afrika Kusini, ambaye alisema: “Kwanza suala la Simba kumuhitaji Shonga bado halijafika kwenye meza yangu, kwa sasa ligi yetu imesimamishwa kwa muda kutokana na mlipuko wa hili janga la Corona.
“Suala la yeye kuongeza mkataba ni kweli tumemuongeza na hakuna timu ambayo inakataa kuuza mchezaji iwapo maslahi yanapokuwa mazuri, ila kwa sasa ni jambo la kusubiri huu wakati upite ili kuweka wazi kila kitu.
Uongozi wa timu ya Orlando Pirates imeweka wazi kuwa ipo tayari kumuachia straika wao, Mzambia, Justin Shonga katika usajili ujao iwapo watafikia muafaka na timu inayomuhitaji.
Mzambia huyo alijiunga na Orlando mwaka 2017 ambapo katika msimu wake wa kwanza alifanikiwa kucheza mechi 19 akifunga mabao manne. Msimu uliopita alifunga mabao sita katika mechi 29.
Post a Comment