PAPY Tshishimbi, kiungo wa Yanga amesema kuwa yupo kwenye mazungumzo na mabosi wake Yanga ili kumalizana nao kuhusu ishu yake ya mkataba.

Tshishimbi kwa sasa mkataba wake ndani ya Yanga umebakiza miezi mitatu na inaelezwa kuwa anafuatwa na timu nyingi ili kupata saini yake.

Tshishimbi amesema kuwa:"Nipo na mazungumzo na Yanga kwa sasa hivyo ikitokea tumekubaliana nao hakuna tatizo nitamwaga wino wangu ili niitumikie Yanga ila kama mambo yatakuwa tofauti basi nitaondoka.

"Kwa sasa bado sijaondoka Yanga kwani mimi ni mali ya Yanga na nitaendelea kuitumikia Yanga mpaka pale mkataba wangu utakapoisha,".

Tshishimbi ndani ya Yanga msimu huu wa 2019/20 akiwa ni nahodha amecheza jumla ya mechi 23 ambazo ni sawa na dakika 2,070 na ametoa pasi moja ya bao amekosa mechi nne kwani Yanga imecheza mechi 27.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.